WritAfrica

HII SERIKALI

By Poet Denkuz

Helloi helloi lama sabaktani
Mungu wangu Mungu wangu mbona unaniacha….
……sssshh……silence
Silence ndo term ma youth walifunzwa before wa learn ku speak out for themselves
But the truth is tulikua na Kenyatta lakini bado hatujapata uhuru
Hii Serikali imekua ya kutenga mabilioni adi imesahau sisi sio bilioni ikaanza kututenga

Mama mboga na watu wa bodaboda pia wametengwa
Wazee wanalalamika vile pesa za uzee zimeadimika
Vijana na stashahada zao wamekosa kazi
Elimu imekua mchezo wa pata potea
Haina maana tena

Wazazi wamechoka, ushuru imepanda, hakuna kulinda mama tena maajabu
Maisha imekua ngumu adi ndugu wa Toka nitoke pia yeye hataki kutoka
Wanasiasa wamekua na matumbo yasiyoshiba shame on you

Kitu hii serikali imefanya ni kuongeza uchumi kwa faida Yao wenyewe,
Sekta ya ukulima imekumbwa na shida chungu mzima
Vijana wamechoka kunyamaza,
There's no more silence in the air
Serikali ya ugatuzi inafyonza Mali ya uma na kijiko

Tumechoka kuwa patient na hakuna dawa kwa mahospitali

Ile uhuru, Dedan kimathi, tom mboya, Jomo, Masinde na wengine wengi walipigania sahii ndo
inapiganiwa,
So sad it's been 60 years since independence lakini bado tuko hapa kama freedom fighters,
Bado tunafight impunity, corruption, na njaa
Niko na too much on my mind just enough to speak out for my country
Siwezi nyamaza tena, we need a proper government to govern us

Ndo tupate change, ni mimi na wewe tuungane pamoja tukiomba Maulana
Like how our anthem says,
O God of all creation
Bless this, our land and nation
Justice be our shield and defender
May we dwell in unity, peace and liberty
Plenty be found within our borders
Amen!

Poet Denkuz

Tags:

No tags assigned to this post.

Related Posts

Top Categories

Trending News

Frozen Future
Kovu cha Kifo
Survival
Death Note
United or Justice
Kiongozi Dhalimu

Subscribe to Our Newsletter

Join our vibrant community of young poets, writers, and illustrators.