WritAfrica

Ahmed Karama

Ahmed Karama

Writer

Ahmed Karama alizaliwa tarehe 17 Aprili 1998 katika jiji la Mombasa, Kenya. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi ya Kengeleni, kisha akaendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Upili ya Baringo Boys. Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi ambako alisomea Uanahabari, akijikita katika taaluma ya mawasiliano, uandishi, na upashanaji habari.

Kwa sasa, Ahmed ni mwanahabari na muandishi mwenye weledi, anayejulikana kwa wepesi wa kufikisha habari kwa njia ya kitaalamu na yenye mvuto. Uandishi wake umejikita katika kutoa maarifa, kukuza uelewa wa jamii, na kuchochea fikra za mabadiliko chanya. Anaamini kuwa kila siku ni fursa ya kujifunza jambo jipya, akifuata falsafa yake ya maisha: "Ishi kwa kujifunza."

Ahmed anaendelea kujijenga kitaaluma huku akijitolea pia kuinua sauti za waliotengwa na kuchangia maendeleo ya kijamii kupitia vyombo vya habari.